Ubuntu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ubuntu
Remove ads

Ubuntu ni falsafa ya Kiafrika inayosisitiza mahusiano na ushirikiano kama msingi wa maisha bora na amani katika jamii. Falsafa hiyo inaonesha nafasi ya mtu katika jamii iliyomzunguka. Ushirikiano ni njia bora ya kuishi kuliko ubinafsi.

Thumb
Sanamu ya tembo yenye mchoro wa Ubuntu, Florianópolis, Brazil.

Neno Ubuntu limetoka kwenye lugha za Kizulu[1] na Kixhosa za Afrika Kusini. Neno la Kihaya "Obuntu" au kwa Kiswahili "Utu" linabeba, kwa kiasi fulani, maana hiyohiyo.

Falsafa ya Ubuntu imetokana na mila na utamaduni wa Kiafrika ambao umejengwa juu ya maslahi ya jamii zaidi ya maslahi ya mtu binafsi [2].

Msingi wa falsafa hiyo ni kamba, "mtu si mtu bila watu" (kwa Kizulu, "Umuntu ngumuntu ngabantu"; kwa Kihaya "Omuntu ti muntu ka ataliho bantu". Baadhi ya watu wanaiona falsafa ya Ubuntu kuwa na maana nzito ya kiroho na ya kidini kwa kuwa imejengwa juu ya upendo kwa watu wengine na hata kwa mazingira.

Remove ads

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads