Uchale

From Wikipedia, the free encyclopedia

Uchale
Remove ads

Uchale (pia undugu wa uchale au undugu wa kuchanjiana) ni undugu unaofanywa kati ya watu wawili ambao hawana undugu wa kuzaliwa kwa kuchanjiana damu.

Thumb
Thomas Heazle Parke akichanjiana na Mwafrika

Mviga wa uchale na sababu zake hutofautiana kulingana na mila na tamaduni za watu wanaofanya undugu namna hiyo[1][2].

Leo, uchale hufanyika katika magenge[3] na baadhi ya vikundi vya uhamasishaji[2].

Kuchanjiana damu kunaweza kueneza maradhi[4].

Remove ads

Utamaduni

Katika jamii za Waafrika ambako uchale ulifanyika, ulitumika kama mkataba[5][6][7] au njia ya kuanzisha uhusiano[8] kati ya wanaume wawili au jamii[6]. Undugu wa aina hii haungevunjika ovyo. Kutoheshimu ndugu wa uchale, kuliaminika kuwa na adhabu ya kiungu[1].

Sababu za kufanya undugu huo zilihusiana wanaume kutaka kulinda mali na kutaka kuhakikisha heshima baina ya ndugu. Kwa mfano, katika jamii za watu wa Kigezi, Uganda, wanaume waliingia katika uchale ili waweze kupitia njia za biashara kwa usalama[7]. Machifu wa jamii za Watio na Wabhobangi walichanjiana ili washirikiane katika raslimali za Mto Kongo[6]. Katika jamii ya Wakikuyu, watu ambao hawakuwa Wakikuyu hawakukubalika hadi wakati mviga wa uchale ufanyike[9][8].

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads