Udadisi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Udadisi
Remove ads

Udadisi (kwa Kiingereza: curiosity, kutoka neno la Kilatini curiositas, yaani "umakini") ni tabia ya kuchunguza kitu au jambo kwa kina[1][2].

Thumb
Watoto Wazungu wa zamani wakidadisi kamera ya Toni Frissell.

Mara nyingi wanasayansi ndio wadadisi wazuri kwa maana wao huchunguza kwa kina na umakini, wakifuata kanuni na kutafuta ushahidi. Kwa njia yao udadisi umestawisha maisha ya binadamu[3].

Katika udadisi kuna ule wa kawaida na mwingine usio wa kawaida. Kwa udadisi wa kawaida mtu hudadisi kwa njia rahisi, tofauti na ule usio wa kawaida ambapo mtu asipokuwa makini anaweza hata kufa. Udadisi huu unahitaji kuwa makini sana.

Udadisi unajitokeza mapema katika mtoto[4], lakini unapozidi na kuelekea mambo yasiyo na maana (kwa mfano umbeya) unamzuia mtu asijue mambo ya maana; hapo ni kilema cha akili.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads