Unestori

From Wikipedia, the free encyclopedia

Unestori
Remove ads

Unestori (kwa Kiingereza Nestorianism[1]) ulikuwa tapo la Ukristo lililofuata mafundisho ya Nestori, mmonaki na mwanateolojia aliyefikia kuwa Patriarki wa Konstantinopoli (leo Istanbul) tangu tarehe 10 Aprili 428 hadi Agosti 431, ambapo kaisari Theodosius II alithibitisha uamuzi dhidi yake uliopitishwa na Mtaguso wa Efeso tarehe 22 Juni.

Thumb
Nestori kadiri ya Romeyn de Hooghe (1688)

Kwa kukataa jina lililozoeleka la Θεοτόκος, Theotokos, "Mama wa Mungu", kwa Bikira Maria, Nestori alisababisha mabishano makubwa na hatimaye mafarakano kuhusu fumbo la Yesu Kristo.

Hasa Sirili wa Aleksandria alimpinga vikali kwa kudai haamini umungu wa Yesu, ingawa mwenyewe alizidi kujitetea hadi kifo chake kwamba anashika imani sahihi.

Matokeo ya mabishano hayo ni Kanisa la Asiria kutengana na Kanisa Katoliki hadi leo, ingawa kwa sasa mafundisho kuhusu Yesu yamelingana.

Remove ads

Tanbihi

Vyanzo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads