Unovisi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Unovisi
Remove ads

Unovisi ni kipindi cha pekee katika malezi ya mashirika ya kitawa. Ni kama kiini chake, na kwa sababu hiyo sheria za Kanisa zinakiratibu kwa uangalifu mkubwa[1].

Aliyejisikia wito, kwanza anaandaliwa miaka au walau miezi ili kuziba mapengo ya malezi ya awali katika familia, shule, parokia n.k. hadi akomae zaidi kiutu na Kikristo.

Ndipo anapoanza unovisi ambao kwa kawaida unachukua miaka miwili au walau mmoja[2]

Wakati huo mhusika anatulia kabisa mbele ya Mungu wake akijaribu maisha ya shirika lake ili kuona kama anayaweza.

Katika hilo ni lazima asaidiwe hasa na mlezi na mafundisho mbalimbali ya kidini: Biblia, liturujia, maisha ya Kiroho, nadhiri n.k.

Akiamua na kukubaliwa, anamaliza unovisi kwa kujitoa kwa Mungu walau kwa mwaka mmoja kabla ya kuweka nadhiri za daima.

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads