Upelaji
From Wikipedia, the free encyclopedia
Upelaji (kwa Kiingereza: Pelagianism) ni mtazamo wa teolojia ya Ukristo unaodhani dhambi ya asili haijaharibu umbile la binadamu, hivyo hiari yake inaweza bado kutekeleza maadili bila kuhitaji neema ya pekee kutoka kwa Mungu. Hatimaye mtu anaweza kujipatia wokovu kwa juhudi zake mwenyewe.

Mtazamo huo umepata jina kutokana na mmonaki wa Ireland[1] Pelagius (354–420 au 440), ingawa pengine huyo alikataa baadhi ya mafundisho yaliyosemekana kuwa yake.
Ulipingwa hasa na Agostino wa Hippo na kulaaniwa na mtaguso wa Kartago wa mwaka 418, halafu na mtaguso wa Efeso (431).
Hata hivyo unajitokeza tena na tena katika historia ya Kanisa, hasa katika makundi yenye juhudi katika maisha ya Kiroho kama upelajiupande.
Tanbihi
Vyanzo
Marejeo mengine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.