Utendi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Utendi (pia: utenzi; kutoka kitenzi "kutenda") ni aina ya ushairi na tanzu mojawapo ya fasihi simulizi. Kwa kawaida, utendi husimulia maisha na matendo ya mhusika shujaa au wa visasili[1].
Maarufu katika fasihi ya Ulaya, kuna tendi kama wimbo wa Troya, wimbo wa Odisei na wimbo wa kabila la Nibelungi; India kuna wimbo wa Mahabharata; Afrika kuna utendi wa Sundiata na wimbo wa Oduduwa. Hizo zote mara nyingi hudondolewa kama mifano ya utendi.
Siku hizi hata riwaya au filamu, hasa kama ni ndefu sana pamoja na wahusika wengi au nyakati nyingi, huitwa utendi.
Kwa Wakristo wanaotumia Kiswahili tahajia "utenzi" inataja hasa nyimbo za kiroho.
Remove ads
Tenzi maarufu za Kiswahili
- Utenzi wa Tambuka (kazi ya Bwana Mwengu, karne ya 18)
- Utenzi wa Shufaka (mtunzi na wakati hawajulikani)
- Utenzi wa Mwana Kupona (kazi ya Mwana Kupona, karne ya 19)
- Utenzi wa Inkishafi (kazi ya Sayyid Abdallah Bin Ally)
- Utendi wa Fumo Liyongo (kazi ya Muhamad Kijumwa)
- Utenzi wa Hayati Sokoine (kazi ya Charles Mloka, karne ya 20)
- Tenzi za Enjili (kazi ya Julius Nyerere)
- Utenzi wa Hati na Adili (Kazi ya Shaaban Robert)
- Mwanangu Nakuusia (kazi ya Audax Kahendaguza Vedasto)
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads