Utomvu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Utomvu ni kiowevu kinachopitishwa katika seli za mimea. Unasafirisha maji na lishe ndani ya mmea[1].


Kutokana na aina mbili tofauti za seli za mimea, yaani zilemu na floemu, kuna aina mbili za utomvu wa zilemu na utomvu wa floemu[2].
Utomvu wa zilemu
Utomvu wa zilemu ni mmumunyo wa maji na homoni, madini na lishe nyingine, Mwendo wake ni kutoka mizizi kuelekea kwenye majani.
Utomvu wa floemu
Utomvu wa floemu ni mmumunyo wa maji na sukari, homoni na madini. Inashuka kutoka sehemu ambako kabohaidreti na sukari zinalishwa kwenda pale zinapohitajika, yaani kwenye sehemu ambako mmea unakua au sehemu ambako kabohaidreti zinatunzwa kama akiba.
Matumizi
Watu wametumia aina za utomvu, hasa ya floemu, tangu kale.
- utomvu wa minazi (na miti mingine ya familia ya Palmae (au: Arecaceae) huwa na sukari nyingi, hutumiwa kutengeza mnazi (aina ya pombe) au pia shira na sukari.
- utomvu wa aina za mikonge umetumika Meksiko sawa na mnazi wa Afrika
- utomvu wa miti ya mipira hutumiwa kutengeneza mpira kwa matairi n.k.
- utomvu wa mibetula hutumiwa na watu wa Urusi na nchi za Baltiki.
- Kanada ni mashuhuri kwa shira kutoka utomvu wa miti ya jenasi Acer (kwa Kiingereza: maple)
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads