Vega
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Vega au α Alfa Lyrae ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Shaliaki (kwa Kiingereza Lyra) na kati ya nyota angavu sana kwenye anga ya usiku.
Jina linatokana na Kiarabu النسر الواقع al-nasr al-waqi, hasa kutoka sehemu ya pili واقع ambamo herufi ya ق q ilichukuliwa kama "g" na hivyo kuleta "Vega" kwa tahajia ya Kilatini. Hili ni jina lililokubaliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia[1].
Vega ni nyota ya safu kuu inayoyeyunganisha hidrojeni kuwa heliamu ndani ya kiini chake. Masi yake ni zaidi ya mara mbili ya masi ya Jua. Ilhali nyota kubwa huchoma fueli yake ya myeyungano haraka kuliko nyota ndogo zaidi Vega itakuwa na maisha mafupi kuliko Jua. Kwa sasa mwangaza halisi ni mara kumi ya Jua. Inazunguka haraka kwenye mhimili wake.
Hadi sasa sayari zinazozunguka Vega hazikuthibitishwa. Lakini kuna dalili ya kwamba kuna mata inayozunguka nyota iliyo katika mchakato ya kujikaza kuwa sayari [2]
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads