Majira ya kupukutika majani
msimu unaofuata baada ya majira ya joto na msimu kabla ya msimu wa baridi From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Majira ya kupukutika majani (kwa Kiingereza Fall au Autumn)[1] ni mojawapo kati ya majira manne ya kanda za wastani, na halijoto yake ni ya baridi kiasi. Kadiri ya umbali na ikweta, mchana unazidi kuwa mfupi na usiku kuwa mrefu.

Pamoja na hayo, miti mingi, isipokuwa misonobari na misanduku, inaweza ikapotewa na majani yote: ndiyo asili ya jina la majira.
Kwa Kiswahili majira ya namna hiyo pia huitwa masika.
Yanafuata majira ya joto (kwa Kiingereza "Summer") na kutangulia majira ya baridi (kwa Kiingereza "Winter").
Majira hayo yanatokea duniani kwa nyakati tofauti kadiri eneo husika lilivyo kaskazini au kusini kwa ikweta. Hata katika nchi ileile, kwa mfano Kenya, majira ni tofauti upande huu na upande huu wa ikweta.
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads