Wagoma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wagoma (kwa Kigoma, au Ki'oma: Ba'ómà) ni kabila la Kibantu kutoka Mkoa wa Kigoma (wilaya ya Kigoma Mjini) na mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (jimbo la Kivu Kusini na wilaya ya Kalemi, eneo ambalo hapo zamani liliitwa Ugoma).
Idadi ya Wagoma haijulikani kwa vile ni kabila la watu wanaopenda kujificha sana na hujitambulisha zaidi kama Wamanyema.[1][2]
Historia
Inasemekana wana asili ya Kaskazini mwa Afrika.
Inaelezwa takribani Wagoma wote walihama eneo la Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa sababu mbalimbali, hususani wakati wa utawala wa Kongo ya Kibelgiji.
Ndilo kabila la kwanza katika makabila ya Kibantu waliowahi kuvuka Ziwa Tanganyika na la mwanzo kuishi eneo la Kigoma Mjini.
Wagoma walifuatiwa na makundi ya Waniakaramba ama Wakwalumona na Wabwari. Kisha Wakwalumona waliunganika miongoni mwa Wabwari na ndipo na wao wakajiita Wabwari na wakakaa Kaskazini mwa Wagoma, kabla yao wote kuhamia na kukaa Ujiji na maeneo yote ya karibu yake ambako hapo wakajiunga na kujiita Wamanyema.
Wagoma waliweza kuvuka kabla ya makundi mengine kwa kufanikiwa kutengeneza mitumbwi ya mti mmoja ambayo waliichonga kutokana na miti ya Mivule iliyokuwa inapatikana Milima ya Goma, Magharibi ya ziwa.
Wagoma huonekana kabila lenye idadi ndogo sana ya watu, kwa sababu watu wake wengi walijiingiza katika makabila mengine kutokana na changamoto nyingi walizokuwa nazo, na miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na mlipuko wa magonjwa ya usingizi. Magonjwa hayo yalisababisha wazee wengi wa familia ya Wagoma kuhamisha familia zao upande wa ujombani kwao, hasahasa katika familia ya Wabondo/Wabembe. Familia hiyo ya Wabembe ndiyo familia ambayo Wagoma waliishi kwa ukaribu nayo sana na pia walioweyana sana na familia ya Wagoma tokea kipindi cha kabla na baada ya ukoloni. Wao Wabembe Waliwaita Wagoma/Bak'yoba.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads