Wamersedari

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wamersedari
Remove ads

Wamersedari ni watawa wa Shirika la Kifalme, la Kimbingu na la Kijeshi la Bikira Maria wa Huruma na la Ukombozi wa Mateka ambalo lilianzishwa na Petro Nolasco mjini Barcelona, mwaka 1218 ili kukomboa Wakristo waliotekwa na Waislamu kama watumwa. [1][2]

Thumb
Logo ya shirika.
Thumb
Basilika la Mercè huko Barcelona lililojengwa lilipokuwepo kanisa mama la shirika mwaka 1267.

Mojawapo kati ya mambo ya pekee ya shirika hilo ni kwamba tangu mwanzo watawa wake wanaweka nadhiri ya nne ya kukubali kufa kwa ajili ya Mkristo aliye katika hatari ya kupoteza imani, kama ilivyokuwa kwa wale waliotekwa utumwani.

Leo shirika linapatikana katika nchi 17.

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads