Petro Nolasco
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Petro Nolasco (kwa Kifaransa Pierre Nolasque; alizaliwa Mas-Saintes-Puelles, Ufaransa, 1189 hivi - Barcelona, leo nchini Hispania, 6 Mei 1256) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki anayekumbukwa hasa kwa juhudi zake za kukomboa Wakristo waliotekwa na Waislamu utumwani pamoja na kurudisha amani [1].

Kwa ajili hiyo alianzisha, pamoja na padri Raimundi wa Penyafort na mfalme Yakobo I wa Aragona, utawa wa Wamersedari naye mwenyewe mwaka 1245 huko Algiers alijitoa kutekwa kwa niaba yao akapigwa hata karibu kufa.
Alitangazwa mtakatifu na Papa Urbano VIII tarehe 30 Septemba 1628.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads