Wastigmatini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wastigmatini (kutoka jina la Shirika la Madonda Matakatifu, ambayo kwa Kilatini yanaitwa Stigmata) ni shirika la kitawa la kikleri la Kanisa Katoliki. Jina rasmi ni Congregatio a Sacris Stigmatibus Domini Nostri Iesus Christi, kifupisho chake ni C.S.S.

Historia
Wastigmatini walianzishwa na mtakatifu Gaspare Bertoni tarehe 4 Novemba 1816 huko Verona, Italia.
Katiba ya kwanza ilifuata kielelezo cha ile ya Wajesuiti iliyoandikwa na Ignas wa Loyola.
Shirika lilikua polepole: mwaka 1905 liliingia Marekani na mwaka 1910 Brazil.
Halafu China, Uthai, Ufilipino na nchi mbalimbali za Afrika (zikiwemo Afrika Kusini, Botswana, Ivory Coast, Tanzania) na Amerika (Kanada na Chile).
Remove ads
Takwimu
Mwaka 2012 walikuwa 422, wakiwemo mapadri 331, katika nyumba 92.
Utume
- kulea vijana
- kuhubiri mafungo na semina
- kusaidia malezi ya kipadri
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads