Wasumbwa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Wasumbwa ni kabila la Watu kutoka eneo la wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita, Kaskazini mwa nchi ya Tanzania.

Mwaka 1987 idadi ya Wasumbwa ilikadiriwa kuwa 191,000[1].

Lugha yao ni Kisumbwa, jamii ya Kisukuma na Kinyamwezi.

Historia

Mtemi wa kabila la Wasumbwa katika eneo la Ushirombo, Kahama, Masumbwe mpaka Lunzewe alikuwa Mtemi Lwassa ambaye alikutwa na utawala wa Wajerumani. Baadaye mtemi Lwassa alikimbilia Upuge, Tabora kwa hofu ya kuuawa na Wajerumani ingawa baada ya Wajerumani kupata taarifa za mtemi Lwassa, utawala uliagiza kumrejesha Kahama ambako ndiyo yalikuwa makao makuu ya Mtemi Lwassa kabla ya kuhamia Lunzewe ambako ndiko alikofariki na kuzikwa katika eneo la musasa runzewe magharibi.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads