Korogwe (mji)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Korogwe ni mji upande wa Kaskazini-Mashariki wa Tanzania ambao ni makao makuu ya Wilaya ya Korogwe. Tangu kupata halmashauri yake ni moja kati ya wilaya 11 za Mkoa wa Tanga kwenye pwani ya Tanzania.
Mwaka 2012 mji ulikuwa na wakazi 68,308 walioishi katika kata 8 za eneo lake.
Mwaka 2012 eneo la mji wa Korogwe lilitengwa na Wilaya ya Korogwe ya awali na kuwa na halmashauri yake ya pekee.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 86,551 [1].
Pia ni makao makuu ya Dayosisi ya Kanisa la Anglikana ya Tanga.
Remove ads
Historia
Korogwe ilianza kama makazi ya kundi la Wasigua (waliojiita pia Waruvu) kwenye kisiwa cha mto Ruvuma. Hapa palikuwa na mkutano wa njia mbili za misafara kutoka Ziwa Viktoria Nyanza na nyingine kutoka Ugogo.
Wakati wa ukoloni wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kulikuwa na kituo cha posta[2], wakati wa koloni ya Tanganyika Korogwe ilikuwa makao makuu ya wilaya [3].
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads