Will Smith

From Wikipedia, the free encyclopedia

Will Smith
Remove ads

Willard Christopher "Will" Smith, Jr. (amezaliwa tar. 25 Septemba 1968)[1] ni mwigizaji, mtayarishaji wa filamu, na rapa kutoka nchini Marekani. Amefurahia sana mafanikio yake ya kimuziki, televisheni na filamu. Gazeti la "Newsweek" limemwita mwigizaji mwenye uwezo mkubwa kabisa duniani.[2] Smith amewahi kushindanishwa kwenye tuzo za Golden Globe mara nne, Academy Awards mara mbili, na ameshinda matuzo kede-kede ya Grammys.

Ukweli wa haraka Amezaliwa, Kazi yake ...

Smith ameanza kujibebea umaarufu akiwa kama rapa chini ya jina la The Fresh Prince mwishoni mwa miaka ua 1980 na jina la uhusika kwenye mfululizo wa televisheni wa The Fresh Prince of Bel-Air. Filamu maarufu ambazo kacheza ni pamoja na Bad Boys na mfululizo wake wa pili Bad Boys II; Men in Black na mfululizo wake wa pili Men in Black II; Independence Day; I, Robot ; Ali; The Pursuit of Happyness; I Am Legend; Hancock; na Seven Pounds. Yeye ni mwigizaji pekee katika historia kuwa na mfululizo wa filamu nane zilizopata mauzo ya dola za Kimarekani milioni 100 kwenye sanduku la ofisi la nyumbani na vilevile kuwa kama mwigizaji pekee kuwa na filamu nane mfululizo kushika nafasi ya kwanza kwenye siku ya uzinduzi wa nyumbani akiwa kama mwigizaji kiongozi.[3]

Remove ads

Familia na maisha ya mwanzoni

Smith, ni Mwafrika-Mwamerika aliyezaliwa na kukulia mjini West Philadelphia na Germantown huko Northwest Philadelphia. Mama yake, Caroline, alikuwa msimamizi wa shule ambaye alifanya kazi kama msimamizi wa bodi ya shule Philadelphia, na baba yake, Willard Christopher Smith, Sr., alikuwa mhandisi wa majokofu.[4][5] Kiimani, alilelewa Kibaptist.[6] Wazazi wake walitengana akiwa na umri wa miaka kumi na tatu na kuja kupeana talaka rasmi akiwa na umri wa miaka thelathini na mbili.[7] Ucheshi wa Smiths na jinsi anavyoonekana akiwa shuleni, wakampa jina la utani kama "Prince", ambalo hatumaye likaja kugeuka na kuwa "Fresh Prince". Wakati yuujanani mwake, Smith akaanza kurao na hatimaye akaanza kushirikiana na Jeff Townes (a.k.a. DJ Jazzy Jeff), ambaye alikutana naye kwenye sherehe moja hivi. Akanza kuhudhuria kwenye shule ya Overbrook High School ya mjini West Philadelphia. DJ Jazzy Jeff & The Fresh Prince ilizaliwa na Smith huku yeye akiimba mistari wakati Townes anashughurikia suala zima la kusugua na kuchanganya midundo—mwungano huo ulikuwa gumzo sana kwenye nyanja za muziki wa hip hop hasa katika miaka ya 1980 na mwazoni mwa 1990.

Remove ads

Diskografia

Makala kuu: Diskografia ya Will Smith
  • Big Willie Style (1997)
  • Willennium (1999)
  • Born to Reign (2002)
  • Lost and Found (2005)

Filmografia

Maelezo zaidi Mwaka, Filamu ...
Remove ads

Soma zaidi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads