Wole Soyinka

Mshindi wa Tuzo ya Nobel Nigeria From Wikipedia, the free encyclopedia

Wole Soyinka
Remove ads

Akinwande Oluwole (au "Wole" Soyinka) ni mwandishi Mnigeria na mshindi Mwafrika wa kwanza wa Tuzo ya Nobel ya fasihi (mwaka wa 1986). Wengi wanamwona ndiye mwandishi bora wa michezo ya kuigizwa Afrika.

Thumb
Wole Soyinka
Thumb

Alizaliwa tarehe 13 Julai 1934 kwa wazazi Wayoruba huko Abeokuta, Nigeria. Alisoma shule ya msingi kwao Abeokuta halafu shule ya sekondari ya Ibadan. Alifuata masomo ya fasihi Chuo Kikuu huko Ibadan (1952-1954) na Leeds (Uingereza) 1954-1957.

Alifundisha fasihi kwenye vyuo vikuu vya Lagos, Ibadan, na Ife.

Soyinka aligongana mara nyingi na serikali za kidikteta za nchi yake akipinga pia udikteta katika nchi mbalimbali kama vile utawala wa Mugabe huko Zimbabwe. Katika maandishi yake alilenga mara nyingi "buti linalokandamiza bila kujali rangi ya mguu ndani yake". Hasa wakati wa udikteta wa jenerali Sani Abacha (1993-1998) Soyinka alijikuta hatarini. Akaondoka Nigeria akaishi nje alipopata nafasi ya profesa ya fasihi kwenye Chuo Kikuu cha Emory (Atlanta - Marekani).

Baada ya mwisho wa utawala wa kijeshi mwaka 1999 Soyinka alikubali nafasi kwenye chuo kikuu cha Ife kwa masharti ya kwamba mwanajeshi mstaafu hatakuwa kamwe chansela wa chuo kikuu kile.

Mwaka 2005 Soyinka ni profesa kwenye chuo kikuu cha Nevada, Marekani.

Wole Soyinka amemwoa mke wake Laide akazaa naye watoto wanne. Aliwahi kuwa na watoto wawili kabla ya kuoa.

Remove ads

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wole Soyinka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads