Zimbabwe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Zimbabwe (jina rasmi: Jamhuri ya Zimbabwe) ni nchi inayopatikana Kusini mwa Afrika, bila pwani, inayopakana na Zambia kaskazini, Msumbiji mashariki, Afrika Kusini kusini, na Botswana magharibi. Ina idadi ya watu takriban milioni 16.7, ikiwa ya 73 duniani. Jiji lake kubwa zaidi na mji mkuu ni Harare. Zimbabwe imegawanyika katika majimbo 10. Inajulikana kwa historia yake ya ustaarabu wa kale, hasa mji wa mawe wa Zimbabwe Kuu, maporomoko maarufu ya Victoria Falls, na historia yake ya kisiasa, ikiwemo utawala wa muda mrefu wa Robert Mugabe na changamoto za kiuchumi zilizoshuhudiwa katika karne ya 21.
Remove ads
Remove ads
Jina
Jina Zimbabwe linatokana na neno "dzimba dzamabwe" linalomaanisha "nyumba ya mawe" kwa lugha ya Kishona. Nyumba hiyo ya mawe, ambayo imehifadhiwa kama eneo la kihistoria, ilikuwa makao ya Ufalme wa Mutapa ambaye mfalme wake aliongoza eneo hilo miaka ya kale.


Eneo
Zimbabwe imegawiwa katika mikoa 8 na miji 2 yenye hadhi ya mikoa. Imegawiwa zaidi katika wilaya 59 na kata 1,200.
- Bulawayo (mji),
- Harare (mji),
- Manicaland,
- Mashonaland ya Kati,
- Mashonaland Mashariki,
- Mashonaland Magharibi,
- Masvingo,
- Matabeleland Kaskazini,
- Matabeleland Kusini na
- Midlands.
Miji minne mikubwa ya Zimbabwe ni:
- Bulawayo, mji wa pili kwa ukubwa
- Harare, mji mkuu
- Chitungwiza
- Mutare


Remove ads
Historia
Historia ya awali
Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.
Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.
Tangu karne ya 11, Zimbabwe ya leo imekuwa na falme imara kwenye njia muhimu ya biashara, hasa ufalme wa Mutapa.
Ukoloni
Kampuni ya British South Africa ya Cecil Rhodes iliweka mipaka ya sasa katika miaka ya 1890.
Koloni la Uingereza lilianzishwa mwaka 1923 kwa jina la Southern Rhodesia.
Mwaka 1965, serikali ya walowezi Wazungu ilijitangazia uhuru kwa jina la Rhodesia tu.
Baada ya miaka 14 ya kutengwa kimataifa na kupigana na raia Waafrika katika miaka ya 1970, mapatano ya mwaka 1979 yalikubali wakazi wote wawe na haki ya kupiga kura na nchi ikawa huru kweli kwa jina la Zimbabwe mwaka 1980.
Baada ya uhuru
Rais Robert Mugabe alipata umaarufu katika siasa kama mpiganaji dhidi ya ukoloni lakini pia kama aina ya dikteta aliyerudisha nyuma uchumi wa nchi.
Baada ya yeye kulazimishwa na wanajeshi kujiuzulu, tarehe 24 Novemba 2017 Emmerson Mnangagwa amekuwa rais mpya wa Zimbabwe.
Demografia
Kabila
Wakazi wengi (82%) ni wa kabila la Washona, 14% ni Wandebele, 2% ni wa makabila mengine ya Kiafrika, 1% ni machotara, Wahindi, Wazungu n.k.
Lugha
Kwa sasa lugha rasmi ni 16. Lugha kubwa ni Kishona (70%) na Kindebele (20%). Kiingereza ni lugha ya kwanza ya chini ya asilimia 2.5% za wakazi.
Dini
Upande wa dini, 84.1% ni Wakristo (hasa Waanglikana, Wakatoliki 8%, Wasabato na Wamethodisti). Waliobaki ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika (4.5%), ni Waislamu (0.7%), au hawana dini (10.2%) .
Remove ads
Tazama pia
- Wilaya za Zimbabwe
- Kata za Zimbabwe
- Orodha ya miji ya Zimbabwe
- Mawasiliano Zimbabwe
- Utamaduni wa Zimbabwe
- Orodha ya lugha za Zimbabwe
- Muziki wa Zimbabwe
- Waandishi wa Zimbabwe
- Mambo ya kigeni Zimbabwe
- Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na msongamano wa watu
- Orodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifa
- Demografia ya Afrika
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads