Yohane Maria Muzei
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Yohane Maria Muzei (Mzee) ni wa mwisho kuuawa kati ya wafiadini wa Uganda wanaoheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu.
Mzaliwa wa eneo la Kagera (katika Tanzania ya leo), alikuwa mtumishi wa kabaka wa Buganda Mwanga II.
Baada ya kumsadiki Yesu Kristo na kubatizwa, alikiri kwa hiari tu imani yake mbele ya waziri mkuu wa mfalme na kwa sababu hiyo alikatwa kichwa huko Mengo tarehe 27 Januari 1887.
Pamoja na wenzake anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Wote pamoja walitangazwa na Papa Benedikto XV kuwa wenye heri tarehe 6 Juni 1920, halafu na Papa Paulo VI kuwa watakatifu tarehe 8 Oktoba 1964.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 3 Juni, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 27 Januari[1].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads