Yosefu Cho Yunho
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Yosefu Cho Yunho (Sinchang, 1848 - Tiyen-Tiyon, 23 Desemba 1866) alikuwa kijana mwenye ndoa wa Korea aliyeuawa kwa ajili ya imani ya Kikristo kama baba yake, Petro Cho Hwaso na babu yake, ila kwa kupigwa fimbo nyingi[1].
Ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.
Huyo na wafiadini wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[2]
Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 23 Desemba[3].
Remove ads
Mazingira
Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[4] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[5].
Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads