Zauditu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Zauditu (pia: Zewditu; ዘውዲቱ [1]; jina la ubatizo: Askala Maryam; 29 Aprili 1876 – 2 Aprili 1930) alikuwa malkia mtawala wa Uhabeshi kuanzia 27 Septemba 1916 hadi kifo chake. Alikuwa mtoto wa kwanza wa Menelik II. Alikuwa kiongozi wa kwanza wa kike wa nchi iliyotambulika kimataifa barani Afrika katika karne ya 19 na 20, na malkia pekee wa Dola la Ethiopia. Yeye ndiye malkia wa hivi karibuni zaidi, pamoja na kuwa kiongozi wa mwisho wa kike wa Ethiopia hadi uchaguzi wa mwaka 2018 wa Sahle-Work Zewde kuwa rais.

Alimfuata Iyasu V. Mwanzoni utawala wake ulisumbuliwa na uasi wa huyo aliyekuwa ameuzuliwa. Malkia huyu anajulikana kwa utegemezi wake mkali kwa utamaduni wa zamani na imani yake kali ya kidini. Jinsi alivyopenda Ukristo ilimfanya mpinzani mkubwa wa mabadiliko aliyokuwa akiyaleta Ras Tafari Makonnen, mrithi aliyeteuliwa, ambaye alikuwa na hisia tofauti kuelekea. Zauditu aligombana sana naye kuhusu mambo ya siasa lakini alishindwa. Naye Tafari alimfuata kama mfalme kwa jina la Haile Selassie.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads