Itikadi kali
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Itikadi kali ni dai la kushikilia sana misimamo ya dini[1][2][3][4][5] au falsafa au siasa fulani kwa kuchukua hasa maneno yaliyoandikwa na mwanzilishi bila ufafanuzi wowote, kadiri unavyohitajika kutokana na muda kupita au mabadiliko mbalimbali kutokea.[6]


Kwa jumla msamiati huu unatumika kwa maana mbaya[7][8], tofauti na mtu kusifiwa kwa uaminifu wake unaoendana na msimamo usio na ukali dhidi ya wengine.
Remove ads
Katika dini
Mfano maarufu wa aina hiyo ni "fundamentalism" iliyoenea katika Uprotestanti huko Marekani katika karne ya 20 ikitaka kushika kabisa mambo 5 ya "msingi" (= fundamentals) kwa kupinga teolojia ya Usasa:
- Biblia kuwa na uvuvio wa Roho Mtakatifu na kwa sababu hiyo kutoweza kukosea hata katika masuala ya sayansi
- Yesu kuwa mzao wa bikira
- Kifo cha Yesu kuwa malipizi ya dhambi za binadamu
- Ufufuko wa Yesu katika mwili wake, si kwa roho tu
- Ukweli wa kihistoria wa miujiza ya Yesu.[9][10]
Mfano mwingine wa siku hizi ni Uislamu wenye itikadi kali kama ule wa DAESH, wa Boko Haram, wa wale wanaolipua hata misikiti, na wa nchi mbalimbali za Kiislamu ambazo zinadhulumu watu wa dini tofauti na hata Waislamu wa madhehebu mengine.
Vilevile dini nyingine kadhaa, kama si zote, zina watu wenye itikadi kali, kama vile Wahindu wanaodhulumu Wahindi wenzao kwa sababu hawafuati dini ya jadi ya India.
Mambo hayo yamefanya wakanamungu na wengineo wadai kwamba dini zote duniani zinaharibu maisha ya watu badala ya kuyaboresha. Watetezi wa dini wanahoji kama ni sawa kusema mwili ni mbaya kwa sababu una ugonjwa katika kiungo fulani. Kwao itikadi kali ni saratani ambayo wote wapambane nayo, badala ya kumuua mtu aliye nayo. Wanasema dini zimechangia sana maadili ya binadamu na ya jamii, hata kama baadhi ya wanadini wameshika misimamo mibaya na kutenda mambo yasiyofaa.
Remove ads
Chanzo na matokeo
Saikolojia na sosholojia zinasaidia kuelewa kwa nini baadhi ya watu wanaelekea kuwa na itikadi kali.
Matokeo ya kawaida ya ukali huo ni kukataa wale wasioamini itikadi yenyewe, lakini pia wale ambao wanaiamini kwa kuifafanua bila ukali.[11]
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads