Efrem wa Syria
From Wikipedia, the free encyclopedia
Efrem wa Siria (kwa Kiaramu: ܐܦܪܝܡ ܣܘܪܝܝܐ, Aphrêm Sûryāyâ; kwa Kiarabu أفرام السرياني; kwa Kigiriki: Ἐφραίμ ὁ Σῦρος, Ephraim Syros; kwa Kilatini: Ephraem Syrus; Nisibi, leo Nusaybin nchini Uturuki, 306 hivi - Edesa, leo Urfa, nchini Uturuki, 9 Juni 373), alikuwa mtawa na shemasi, mwanateolojia na mwanashairi pamoja.
Ni maarufu hasa kwa tenzi zake nyingi ajabu kwa lugha ya Kiaramu ambazo zinatumika hadi leo katika liturujia na kutokeza imani kwa namna bora.
Ndiye mwakilishi muhimu zaidi wa Ukristo wa Kisiria.
Kisha kufa akaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu na babu wa Kanisa.
Papa Benedikto XV tarehe 5 Oktoba 1920 alimuongezea sifa ya mwalimu wa Kanisa.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe ya kifo chake[1].