From Wikipedia, the free encyclopedia
John David Jackson (amezaliwa tar. 18 Novemba 1977) ni msanii wa rekodi za hip hop kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Fabolous. Alikulia mjini Brooklyn huko New York City, alikuwa mmoja kati marapa wa East Coast ambao waliathiriwa na muziki wa Southern hip hop. Moja kati ya kazi zake za awali ambayo ilimletea umaarufu ni pamoja na "Can't Deny It" mnamo 2001, kutoka katika albamu yake ya kwanza ya Ghetto Fabolous. Fabolous ametoa albamu tano, ambazo zote kwa ujumla zimeuza nakala zaidi ya milioni tatu huko nchini Marekani.[1]
Fabolous | |
---|---|
Fabolous at Sirius Satellite Radio in 2007 | |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | John David Jackson |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Rapa, mtunzi wa nyimbo |
Miaka ya kazi | 1998–mpaka sasa |
Studio | Desert Storm, Def Jam |
Ame/Wameshirikiana na | Jagged Edge, Lil Mo, Nate Dogg, Mike Shorey, Ne-Yo, Pharrell Williams, Red Cafe, The-Dream, Young Jeezy |
Fabolous alizaliwa John David Jackson mnamo tar. 18 Novemba 1977, na wazazi wenye asili ya Kiafrika-Kiamerika na Kidominika.[2][3] Alikulia huko Bedford-Stuyvesant jirani kidogo na Brooklyn, New York.[4][5] Wakati anasoma elimu ya juu, Fabolous akaanza kujifua katika masuala ya muziki wa rap. Alialikwa kurap moja kwa moja kipindi cha redio cha DJ Clue na kwenye WQHT Hot 97, ambapo kulimpatia uwezo wa kuweza kuingia mkataba na studio ya Desert Storm Records.[6] Alipata kushirikishwa kwenye mamixi tepu kibao ya DJ Clue na mamixi tepu mengine mingi tu ya wasaniii wa Roc-A-Fella.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.