From Wikipedia, the free encyclopedia
Floriani wa Lorch (alifia dini tarehe 4 Mei 304) alikuwa askari Mkristo wa Dola la Roma aliyeishi Mantem, karibu na Kirchdorf an der Krems, leo nchini Austria.
Aliposikia kwamba gavana Akwilino, wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano, amekamata Wakristo 40 mjini Lorch, alitamani kuwa nao akaenda huko. Karibu na kufika alikutana na askari wenzake akajitambulisha kuwa Mkristo, hivyo akakamatwa na kupelekwa kwa Akwilino. Huyo alijaribu kumfanya atoe sadaka kwa miungu, lakini Floriani alipokataa aliagiza apigwe mijeledi na kutupwa katika mto Enns akiwa na jiwe kubwa limefungwa shingoni[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.