From Wikipedia, the free encyclopedia
Kaunti ya Kirinyaga ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Kaunti ya Kirinyaga | |||
---|---|---|---|
Kaunti | |||
Vijana wakilima katika mradi wa umwagiliaji wa Mwea | |||
| |||
Kirinyaga County in Kenya.svg Kaunti ya Kirinyaga katika Kenya | |||
Nchi | Kenya | ||
Namba | 20 | ||
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 | ||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Kati | ||
Makao Makuu | Kutus(Rasmi) | ||
Miji mingine | Kerugoya, Sagana, Wang'uru | ||
Gavana | Anne Mumbi Waiguru | ||
Naibu wa Gavana | Peter Njagi Ndambiri | ||
Seneta | Daniel Karaba Dickson | ||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Purity Wangui Ngirici | ||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Kirinyaga | ||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 20 | ||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 4 | ||
Eneo | km2 1 478.3 (sq mi 570.8) | ||
Idadi ya watu | 610,411 | ||
Wiani wa idadi ya watu | 413 | ||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||
Tovuti | kirinyaga.go.ke |
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 610,411 katika eneo la km2 1,478.3, msongamano ukiwa hivyo wa watu 413 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu yako Kerugoya/Kutus.
Kaunti ya Kirinyaga imepakana na Nyeri (magharibi), Murang'a (kusini magharibi) na Embu (mashariki).
Mlima kenya na msitu unaouzunguka uko kaskazini mwa kaunti. Theluji ambayo huyeyuka kutoka Mlima Kenya hutengeneza mito, k.v. Mto Thiba na Mto Kiganjo. Mito mingine iliyo katika kaunti hii ni Mto Sagana, Mto Nyamindi, Mto Rupingazi, Mto Thiba, Mto Rwamuthambi and Mto Ragati[2].
Kirinyaga huwa na tabianchi tropiki na hupata misimu miwili ya mvua.
Kaunti ya Kirinyaga imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[3]:
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.