From Wikipedia, the free encyclopedia
Marko wa Efeso (jina la awali: Manuel Eugenikos; Konstantinopoli, 1392 - Konstantinopoli, 23 Juni 1444) alikuwa mmonaki, mshairi[1] na mwanateolojia wa Kiorthodoksi kutoka Dola la Bizanti na askofu mkuu wa Efeso.
Alipata umaarufu kwa kushiriki katika Mtaguso wa Ferrara-Florence (1438–1439) na kushika msimamo mkali zaidi dhidi ya madai ya Kanisa Katoliki kwa ajili ya muungano.
Mwaka 1734 alitangazwa na Patriarki Serafim I wa Konstantinopoli pamoja na sinodi yake kuwa mtakatifu.
Aliacha maandishi mengi, yakiwemo ya tenzi, vitabu vya teolojia, anthropolojia n.k.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.