Mileto
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mileto (kwa Kigiriki Μῑ́λητος, Mīlētos) kuanzia mwaka 1000 KK hivi ulikuwa mji wa Wayunani huko Karia kwenye mto Meandro unapoishia katika Bahari ya Kati, kwenye pwani ya Uturuki wa leo, karibu na kijiji cha Balat.
Kabla ya uvamizi wa Wapersia katikati ya karne ya 6 KK ulitajwa kuwa mkubwa na tajiri kuliko miji yote ya Wagiriki.
Maghofu yake ni kati ya mahali muhimu pa akiolojia[1][2][3][4][5][6].
Mtume Paulo alifika huko mwaka 58 akakutana na viongozi wa Kanisa la mji jirani, Efeso (Mdo 20:15–38), ambapo alikaa miaka mitatu na kutoka huko alieneza Ukristo katika mkoa mzima wa Asia (Mdo 19:10, 20; 1Kor 16:9).
Inawezekana alirudi tena huko miaka 65-66 kwa kuwa aliandika kwamba aliacha huko Trofimo (2Tim 4:20), na si katika safari ile ya kwanza (Mdo 21:29).