Nabii Ahiya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nabii Ahiya (kwa Kiebrania: אחיה השילוני, Aḥiyah[1] "YHWH ni ndugu yangu"[2]) alikuwa nabii wa kabila la Lawi kutoka Shilo wakati wa mfalme Solomoni, inavyoelezwa na Biblia ya Kiebrania (Kitabu cha kwanza cha Wafalme).
Ahiya ni maarufu hasa kwa kuwa alimtabiri Yeroboamu kwamba atakuwa mfalme wa makabila kumi wa Israeli Kaskazini (1Fal 11:29-39)[3].
Baadaye alimtabiria mke wa Yeroboamu I kifo cha mwanae na maangamizi ya ukoo wake pamoja na uhamisho wa Israeli hadi ng'ambo ya mto Eufrate (1Fal 14:6-16)[4].
Kadiri ya Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati, Ahiya alitunga pia kitabu chenye jina la "Unabii wa Ahiya wa Shilo" na taarifa kuhusu ufalme wa Solomoni (2Nya 9:29). Hata hivyo kitabu hicho hakijatufikia. Katika 1Fal 11:41 kinaitwa "Matendo ya Solomoni".