From Wikipedia, the free encyclopedia
Niklas Zennström (alizaliwa 16 Februari 1966) ni bilionea mjasiriamali wa Uswidi anayejulikana zaidi kwa kuanzisha kampuni mbalimbali za intaneti akishirikiana na Janus Friis zikiwemo Skype na Kazaa. Hivi karibuni alianzisha kampuni ya uwekezaji ya Atomico.
Zennström pia ni mmoja wa waanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Zennström Philanthropies.
Zennström ana shahada toka Chuo Kikuu cha Uppsala na KTH Royal Institute of Technology.
Zennström alianza kazi mwaka 1991 kwenye shirika la simu la Tele2. Aliwahi pia kuwa mkurugenzi wa kampuni ya everyday.com.
Mwaka 2000 Zennström na Janus Friis walianzisha Kazaa. Baada ya wanamuziki na watoa filamu nchini Marekani kufungua kesi dhidi ya Kazaa, kampuni hii ilinunuliwa na Sharman Networks.
Baadaye Zennström alianzisha kampuni ya Joltid na Altnet.
Mafanikio makubwa ya Zennström hadi leo ni kampuni ya Skype. Oktoba 2005 Skype ilinunuliwa na eBay kwa pauni bilioni 2.1. Zennström alikuwa mkurugenzi wa Skype hadi Septemba 2007. Baada ya kuuza Skype, Zennström alianzisha kampuni ya Joost, huduma ya kusambaza video kwenye intaneti, mwaka 2007.
Mwaka 2009 Zennström alikuwa mmoja wa wawekezaji walionunua Skype Technologies toka kwa eBay. Hivi sasa, Zennström anaongoza kampuni ya Atomico. Kampuni hii, yenye makao yake makuu nchini Uingereza inawekeza kwenye kampuni za teknolojia zinazokua kwa kasi. KupitiaAtomico wamewekeza kwenye zaidi ya kampuni 50 kwenye mabara manne zikiwemo kampuni za Supercell, Rovio, Last.fm, Fon, Rdio, Fab, Klarna na Skype.
Mei 2011 Skype ilinunuliwa na Microsoft kwa dola bilioni 8.5. Inaaminika kuwa Zennström na Friis walijipatia dola bilioni 1.[1]
Novemba 2014 Zennström aliingizwa kwenye SUP46's Swedish Startup Hall of Fame.[2]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.