Uswidi
nchi katika Ulaya Kaskazini From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Uswidi, rasmi kama Ufalme wa Uswidi, ni nchi iliyoko kaskazini mwa Ulaya kwenye Rasi ya Scandinavia. Inapakana na Norwei upande wa magharibi, Ufini upande wa kaskazini-mashariki, na imetenganishwa na Udeni upande wa kusini kwa Mlango wa Bahari ya Öresund. Ikiwa na idadi ya watu wapatao milioni 10.5, inashika nafasi ya 88 kwa idadi ya watu duniani. Stockholm ndiyo mji mkuu na jiji kubwa zaidi la Uswidi.
Remove ads
Uswidi ni taifa lenye historia ndefu ya kifalme na utawala wa kikatiba, ambapo mfalme hutumikia zaidi kama ishara ya kitaifa kuliko kuwa na mamlaka ya moja kwa moja kisiasa. Bunge lake linaitwa Riksdag, na lina wajibu wa kutunga sheria na kusimamia serikali. Uswidi inajivunia utawala wa kidemokrasia, uhuru wa vyombo vya habari, na haki za binadamu, na imekuwa mfano wa maendeleo ya kijamii na kisiasa katika bara la Ulaya.
Kiuchumi, Uswidi ni mojawapo ya nchi zilizoendelea zaidi duniani, ikiwa na uchumi unaotegemea viwanda vya kisasa, teknolojia, na huduma. Kampuni kubwa kama Volvo, Ericsson, na IKEA zina asili ya Kiswidi. Aidha, Uswidi inatambulika kwa mifumo ya kijamii inayotoa huduma bora za afya, elimu isiyolipiwa hadi kiwango cha juu, na usawa wa kijinsia. Mazingira yake ya asili yanajumuisha misitu mikubwa, maziwa mengi, na majira marefu ya baridi, hali inayoifanya kuwa kivutio kikubwa cha utalii wa asili.
Remove ads
Jiografia
Nchi imegawiwa katika mikoa mitatu: Norrland katika kaskazini, Svealand katikati na Götaland katika kusini.
Ina pwani ndefu kwenye bahari ya Baltiki. Kuna daraja la kuvukia mlango wa bahari ya Oresund ya kuunganisha Uswidi na Denmark.
Kuna misitu mikubwa sana na maziwa mengi.
Hali ya hewa ya sehemu kubwa ya Uswidi si baridi kutokana na athira ya mkondo wa Ghuba. Kuna tofauti kati ya urefu wa mchana katika miezi ya Mei hadi Julai na giza wakati wa Desemba. Tarehe 21 Juni ni siku ndefu: hakuna giza kabisa na usiku wake Waswidi hufanya sherehe kubwa ya "midsommar" kwa ngoma na dansi kote nchini.
Mji mkuu ni Stockholm, nao unaongoza kwa wingi wa wakazi.
Milima na vilele
Vilele vya juu kwa kila "landskap" ni kama ifuatavyo. Kumbuka kwamba "landskap" katika Uswidi ni sahihi kidogo tu. Basi maoni mengine kuwepo.
Remove ads
Wilaya
Remove ads
Historia
Wakazi wa kwanza kujilikana walikuwa makabila ya Kijerumaniki kama wakazi wote waliowafuata. Huko Roma Tacitus aliandika juu yao mwaka 98 BK.
Kati ya karne ya 8 hadi ya 11 waliitwa mara nyingi "Waviking" wakiogopwa na wenyeji wa Ulaya bara kwa sababu Waviking walivamia mara kwa mara maeneo ya pwani kwa jahazi zao ndogo. Lakini Waviking au Wanormani ni neno la kutaja watu wa Kaskazini waliovamia na kufanya ujambazi kwenye nchi za Ulaya bara si namna jinsi wenyewe walivyojiita.
Malkia Margarete I wa Udani aliolewa na mfalme wa Norway. Baada ya kifo cha mumewe alitawala nchi zote mbili na baadaye pia Uswidi. Mwaka 1397 wawakilishi wa falme tatu zilikutana katika mji wa Kalmar (Uswidi ya kusini) na kuelewana juu ya "Umoja wa Kalmar" yaliyounganisha nchi zote za Skandinavia chini ya mfalme wa Denmark ilhali kila nchi iliendelea kujitawala. Wakati ule Ufini (Finland) ilikuwa chini ya Uswidi. Iceland na Visiwa vya Faroe ziliingia pia kwa sababu zilikuwa chini ya Norway wakati ule.
Umoja huo uliendela hadi mwaka 1521. Waswidi walianza kuchoka na utawala wa Kidenmark wakaondoka katika umoja huu mwaka 1521 pamoja na Ufini. Lakini Norway iliendela kuwa chini ya Denmark hadi mwaka 1814.
Uswidi ulijiunga na Matengenezo ya Kiprotestanti na kanisa la Kilutheri likawa dini rasmi nchini hadi mwaka 2000. Hivyo Uswidi ikawa kati ya nchi muhimu sana ya Ulutheri.
Uswidi ulistawi na kueneza himaya yake kuanzia karne ya 17 hadi mwanzo wa karne ya 18 kama mojawapo kati ya nchi zenye nguvu zaidi Ulaya.
Baadaye ilirudi nyuma hadi kunyang'anywa kwa Ufini na Warusi (1809).
Kati ya miaka 1814 na 1905 ililazimisha Norwei kukubali mfalme wa Uswidi kama mfalme wa Norwei pia.
Tangu hapo Uswidi umeshika msimamo wa amani na wa kutoshikamana na nchi yoyote.
Kwa sasa Uswidi ni ufalme wa kikatiba yaani Mkuu wa Dola ni mfalme (kwa sasa Carl XVI Gustaf), lakini huyu mfalme anapaswa kufuata sheria ya katiba ya nchi. Utawala umo mikononi mwa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.
Katika karne ya 20 Uswidi umefaulu vizuri kujenga uchumi ili kuondoka katika umaskini na kuwa moja kati ya nchi tajiri za dunia (ikiwa na nafasi ya 8 kwa pato la kichwa).
Nchi ilijiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 1995 lakini haikukubali pesa ya Euro ikaendelea na Krona ya Uswidi.
Remove ads
Watu
Uswidi ni nchi kubwa yenye wakazi wachache: mwaka 2017 kwa mara ya kwanza wamezidi milioni 10, wengi wao wenye asili ya makabila ya Kijerumani, lakini kwa sasa 32.2% wana damu tofauti au mchanganyiko.
Lugha rasmi ni Kiswidi, ambacho kinafanana sana na Kidani na Kinorwe. Lugha ya pili kati ya tano zilizokubalika kwa makundi madogo ya asili ni Kifini (5%), lakini siku hizi uhamiaji umefanya Kiarabu kiwe na watumiaji wengi zaidi.
Asilimia 89 wanaweza kuongea Kiingereza pia.
Upande wa dini, 57.7% ni Walutheri, lakini kati yao 2% tu wanashiriki ibada ya kila wiki. Waprotestanti wengine ni 275,000, Waorthodoksi wa Mashariki 100,000 na Wakatoliki 92,000.
Waislamu ni kama 600,000, lakini wengi hawashiriki, na 25,000 tu wanafuata swala tano.
Remove ads
Picha
- Kebnekaise ni mlima mkubwa wa Uswidi
- Ziwa la Vänern
- Wanyamapori wakubwa wa Uswidi ni mbawala wakubwa
- Stockholm – mji wa kale
- Migodi ya Kiruna
Tazama pia
Viungo vya nje
- Sweden entry at The World Factbook
- Sweden entry at Encyclopædia Britannica
- Sweden Ilihifadhiwa 25 Januari 2009 kwenye Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Uswidi katika Open Directory Project
- Sweden profile from the BBC News
- Wikimedia Atlas of Sweden
- Key Development Forecasts for Sweden from International Futures
- Study in Sweden – Official guide to studying in Sweden
- Ilihifadhiwa 30 Desemba 2014 kwenye Wayback Machine. Technological Waves and Economic Growth in Sweden 1850–2005
- Sweden – Economic Growth and Structural Change, 1800–2000 — EH.Net Encyclopedia
- vifanord – A digital library that provides scientific information on the Nordic and Baltic countries as well as the Baltic region as a whole
- Tovuti rasmi
- Sweden.se — Sweden's official portal
- The Swedish Parliament – Official website
- The Government of Sweden – Official website
- The Royal Court Ilihifadhiwa 11 Oktoba 2016 kwenye Wayback Machine. – Official website of the Swedish Monarchy
- Habari
- Radio Sweden – Public service
- Sveriges Television (Kiswidi) – Public service
- Dagens Nyheter (Kiswidi)
- Svenska Dagbladet (Kiswidi)
- The Local – Sweden's news in English – Independent English language news site
- Biashara
- Utalii
- VisitSweden.com – Official travel and tourism website for Sweden
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Uswidi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads