Yasinto wa Krakau
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yasinto wa Krakau, O.P. (kwa Kipolandi: Jacek Odrowąż; 1185 - 15 Agosti 1257) alikuwa padri kanoni wa Polandi ambaye alipokutana na Dominiko wa Guzman huko Bologna (Italia) alijiunga na shirika lake jipya.
Baadaye alitumwa kulieneza katika Ulaya Mashariki (Polandi na Ukraina) akahubiri Injili hata Bohemia na Silesia [1].
Papa Klementi VIII alimtangaza mtakatifu mwaka 1594.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Agosti[2], lakini pia 17 Agosti.