Yusto Ranfer
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yusto Ranfer, M.E.P. (Chalon-sur-Saône, Saône-et-Loire, Ufaransa, 28 Februari 1838 - Sai-Nam-Hte, 7 Machi 1866) ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.
Padri huyo mmisionari alikatwa kichwa pamoja na askofu Simeoni-Fransisko Berneux na mapadri wawili wa shirika lake: Alois Beaulieu na Petro-Henri Dorie kwa sababu, walipoulizwa na watesi wamefika Korea kufanya nini, walijibu kwa ujasiri na unyofu kwamba wana lengo la kuokoa watu kwa jina la Yesu[1].
Hao na wafiadini wenzao 99 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[2]
Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba.