Adrian Atiman
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Adrian Atiman (Tindirma, Sudan ya Kifaransa, leo Mali, 1866 hivi [1] - Karema, mkoa wa Katavi, 24 Aprili 1956[2]) alikuwa katekista na daktari wa Kiafrika mmisionari nchini Tanzania[3].
Maisha
Msonghai, alikombolewa na Wamisionari wa Afrika kutoka utumwa huko Metlili, kusini mwa Algeria[4].
Baada ya kusomeshwa hadi Ulaya[1] aliishi na kufanya kazi katika misheni ya Karema kuanzia mwaka 1889[5] hadi kifo chake akiheshimiwa na wote[2] kwa huduma zake zilizomfikisha hata vijiji vya mbali[2].
Aliacha mke na mtoto mmoja, padri Joseph[5], pamoja na masimulizi ya maisha yake.[6]
Tanbihi
Marejeo kwa Kiswahili
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads