Mkoa wa Katavi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mkoa wa Katavi ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Ulianzishwa rasmi mnamo Machi 2012 kwa kumega sehemu ya kaskazini ya mkoa wa Rukwa. Unapakana pia na mkoa wa Tabora upande wa mashariki na mkoa wa Songwe upande wa kusini. Eneo lake ni la km2 45,843 mashariki mwa ziwa Tanganyika. Katika sensa ya mwaka 2022 idadi ya wakazi ilihesabiwa kuwa 1,152,958 [1]. Makao makuu yako Mpanda.
Remove ads
Wilaya
Wilaya za mkoa huo ni tano tu: Mlele, Nsimbo, Mpanda mjini, Tanganyika (awali Mpanda vijijini) na Mpimbwe.
Utamaduni
Kabila kubwa ni lile la Wafipa; pia kuna Wabende, Wapimbwe na Wakonongo na dini yao kwa kiasi kikubwa sana ni Ukristo wa madhehebu ya Kanisa Katoliki.
Wapimbwe wanapatikana katika maeneo ya wilaya ya Mpimbwe katika vijiji vya Mamba, Mpimbwe na Majimoto. Katika kijiji cha Mamba kuna kivutio kizuri: bwawa kubwa la asili la maji ya moto ambayo hayapoi muda wote, ni ya moto iwe mchana au usiku.
Pia kuna sehemu za mkoa huu ni wa kihistoria katika baadhi ya maeneo. Mfano mtaa wa Madukani ambao walikua wakiishi Wahindi na Waarabu wa Oman kama Mzee Yusuf Al Salmi.
Remove ads
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
Tazama pia
Marejeo
Viungo vya nje
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads