Afande Sele

Mwanamuziki wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Afande Sele (jina halisi: Seleman Msindi; alizaliwa 24 Aprili 1976) ni msanii wa muziki wa hip hop na Bongo Flava kutoka Mkoani Morogoro, Tanzania. Amewahi kushinda tuzo ya (mkali wa ryhmes) mwaka 2003 kutokana na wimbo wake wa "Darubini Kali" aliyomshirikisha Dogo Ditto kwa sasa Lameck Ditto. Ni muasisi wa makundi ya 'Ghetto Boys' na 'Watu Pori' yaliyoanzishwa na kufia mjini Morogoro kwa kuongozana na alikuwa msanii wa kwanza kuujaza uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri mjini Morogoro alipozindua albamu yake ya kwanza ya 'Mkuki Moyoni'.[1] Aliongoza kampeni ya malaria mwanzoni mwa miaka ya 2005 na 2007.

Ukweli wa haraka Jina la kuzaliwa, Amezaliwa ...

Mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka 2012 alitangaza rasmi kufanya kazi kama kundi jipya la watu pori baada ya kufanya kazi na MC KOBA ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wakiunda kundi la watu pori miaka ya nyuma. Ametoa nyimbo nyingi kali zikiwemo MtazamoO, Amani na Upendo, Simba Dume na nyingine nyingi. Afande Sele kwa sasa ana video ya wimbo wake Soma Ule ambayo imeongozwa na mtayarishaji Raph Tz (upcoming video director) aliyepewa heshima na msanii huyo kufanya video hiyo ambayo imekidhi maudhui ya wimbo.

Remove ads

Maisha Binafsi

Afande Sele ana watoto wawili wa kike, Tunda na Sanaa wanaoishi huko mkoani Morogoro. Afande Sele alifiwa na mkewe Asha (Mama Tunda) mnamo Agosti 14, 2014. Kwa sasa Tunda anasoma sekondari iitwayo Charlotte iliyopo maeneo ya Nanenane, mjini Morogoro.

Afande Sele alijiunga na chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT) ambacho kiliongozwa na aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Zuberi Kabwe, akitokea vilevile CHADEMA. Huku nako hakudumu sana akajivua uanachama wake na kuhamia Chama cha Mapinduzi.[2]

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads