Chama cha Mapinduzi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Chama Cha Mapinduzi (kifupi: CCM) ndicho chama tawala cha kisiasa nchini Tanzania, kilichoanzishwa tarehe 5 Februari 1977 kupitia muungano wa vyama viwili: Tanganyika African National Union (TANU) kutoka bara, chini ya uongozi wa Julius Nyerere, na Afro-Shirazi Party (ASP) kutoka Zanzibar, kilichokuwa na nguvu visiwani. Muungano huo uliashiria hatua muhimu ya kuimarisha mshikamano kati ya maeneo ya Tanzania bara na visiwani, kwa lengo la kuunda chama kimoja kitakachoiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha mfumo wa chama kimoja.

Tangu kuanzishwa kwake, CCM imeendelea kuwa nguvu kuu katika siasa za Tanzania. Hata baada ya kurejea kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, chama hicho kimekuwa kikishinda uchaguzi mkuu kwa uendelevu, kikitoa marais wote wa Muungano na wa Zanzibar. Kinaendelea kudhibiti viti vingi vya Bunge pamoja na serikali nyingi za mitaa nchini. Ingawa upinzani umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni, CCM bado kina unadhibiti kwa nguvu za dola mwelekeo wa kisiasa na sera za nchi.
Remove ads
Historia
CCM ilizaliwa tarehe 5 Februari 1977 baada ya kuungana kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala cha Zanzibar wakati huo. Chama cha TANU kilikuwa kikiongozwa na Mwalimu Nyerere na Afro-Shiraz Party kilikuwa chini ya Amaan Karume.
Itikadi

Kwa miaka mingi CCM ilikuwa ikifuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Itikadi hii ilipewa nguvu za kisera mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la Arusha.
Kutokana na azimio hilo uchumi uliwekwa mikononi mwa umma. Itikadi hiyo pia ilisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja hasa katika vijiji vya Ujamaa.
Uchaguzi
CCM imekuwa ikishinda chaguzi za Urais toka mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa nchini Tanzania.
Chama hicho kimekuwa pia kikipata idadi kubwa ya wabunge wa Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi, ingawa vyama vya upinzani vilitoa malalamiko kuhusu utekelezaji wa haki na uchakachuaji wa kura.
Chaguzi za vyama vingi Tanzania baada ya kurejeshwa kwa mfumo huo zilifanyika mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010 na viongozi walioweza kuwa washindi kakati chama hicho ni kama wafuatao: Benjamin Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete. Hawa ndio watu waliongoza nchi kipindi cha miaka ishirini.
Katika historia ya CCM kumekuwa na wenyeviti watano:
- Julius Nyerere, 1977 - 1990,
- Ali Hassan Mwinyi 1990 - 1996
- Benjamin Mkapa 1996 - 2006,
- Jakaya Kikwete 2006 - 2016
- John Pombe Magufuli 2016 - 2021
- Samia Suluhu Hassan 2021 hadi sasa
Viungo vya nje
- Tovuti ya Chama cha Mapinduzi
- Ukurasa wa Facebook wa Chama cha Mapinduzi
- Ukurasa wa Twitter wa Chama cha Mapinduzi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads