Ajali
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ajali (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: "accident" au "uninentional injury") ni tukio maalumu linalotambulika na lisilotarajiwa, geni na lisilotakikana ambalo hutokea katika muda na mahali fulani bila sababu au makusudi dhahiri, lakini husababisha madhara yaliyo wazi, hasa vifo.
Ajali hudokeza kwa ujumla matokeo mabaya ambayo labda yangeweza kuepukwa au kukingwa ikiwa matukio yaliyosababisha ajali hiyo yangetambuliwa na kurekebishwa kabla ya tukio hilo.
Wataalamu katika nyanja za kuepuka majeraha hawatumii neno 'ajali' kuelezea matukio ambayo husababisha majeraha katika jaribio la kubainisha asili ya majeraha mengi ambayo yangeweza kukingwa. Matukio kama hayo huzingatiwa kutoka mtazamo wa epidemiolojia - yanaweza kuepukwa na kukingwa. Maneno yanayopendelewa huweza kulifananua tukio lenyewe zaidi, badala ya asili yake isiyotakikana (k.m kugongana, kufa maji, kuanguka, n.k)
Ajali ya aina ya kawaida (magari, moto, n.k.) huchunguzwa ili kubaini jinsi ya kuepukana nazo katika siku zijazo. Mara nyingine hii hujulikana kama uchambuzi wa sababu ya asili, lakini haihusu ajali ambazo haziwezi kutabiriwa. Sababu haswa ya ajali ya nadra isiyoweza kuepukwa huenda ikawa haiwezi tambulika, na hivyo matukio ya siku zijazo yatabaki kuwa "ajali."
Ufafanuzi
Unapofafanua kinaganaga, ajali huweza kutaja tukio lenyewe pekee, bila kuzingatia mazingira ya tukio hilo, au athari za tukio hilo, yaani "ajali" huishia katika tukio la mara moja, ambalo huleta athari ambazo hazikutarajiwa.
Hata hivyo, katika matumizi ya kawaida, 'ajali' huenda ni pamoja na mfumo mzima wa mazingira (fursa, iliyokuwepo awali, au matokeo yanayojiendeleza bila kuthibitishwa; matokeo ya kawaida; wakati na mahali yasiyoweza kutabiriwa; washiriki n.k.) yanayoelekea, pamoja na kusababishwa na tukio hilo.
Aina

107-247 248-287 288-338 339-387 388-436 437-505 506-574 575-655 656-834 835-1,165
Kimaungo na yasiyo ya kimaungo
Mifano ya kimaungo ni kama migongano isiyotarajiwa au maanguko, kujeruhiwa kwa kugusa kitu kikali, moto, au umeme, au kunywa sumu.
Mifano ya ajali isiyo ya kimaungo ni kama kutoboa siri bila kutaka au kusema kitu kimakosa, kusahau miadi, n.k.
Katika shughuli
- Ajali wakati wa utekelezaji wa kazi huitwa ajali kazini.
- Kwa kulinganisha, ajali zinazotupata tukibarizi au tunapostarehe huwa sanasana ni majeraha ya michezo.
Kwa vyombo vya usafiri
Tunatakiwa tuendeshe vyombo vya usafiri kwa uangalifu ili kupunguza ajali, kama vile:
- Ajali ya baiskeli
- Ajali ya pikipiki
- Ajali ya magari
- Ajali ya meli
- Ajali ya reli
Sababu za kawaida

Kwa majeraha ya kimwili yanayopeleka watu kulazwa hospitalini, nyingi huwa ni ajali za barabarani na kuanguka.
Tazama pia
- Jeraha
- Uwezekano wa ajali
- Usalama angani
- Orodha ya ajali za ndege
- Baiskeli
- Ajali ya baiskeli
- Usalama wa baiskeli
- Pikipiki
- Ajali ya pikipiki
- Gari
- Ajali ya gari
- Usalama wa gari
- Reli
- Ajali ya reli
- Orodha ya ajali za reli
- Ajali ya kinyuklia
- Orodha ya ajali za kinyuklia
- Usimamizi wa hatari
- Meli
- Ajali za meli
- Usalama
- Uhandisi wa usalama
- Usalama kazini
- Nguo za kujikinga na ajali
- Taaluma ya afya na usalama kazini
- Uchambuzi wa ajali
Viungo vya nje
- Ajali Ilihifadhiwa 16 Agosti 2013 kwenye Wayback Machine. (Kuumia kibinafsi na uganga mbaya)
- Ajali za kijamii katika barabara za Ulaya Ilihifadhiwa 28 Aprili 2006 kwenye Wayback Machine. (CARE)
- Uko na Usalama Ilihifadhiwa 9 Januari 2019 kwenye Wayback Machine. (Vidokezo na maelezo ya usalama)
- Ajali ya magari tovuti rasmi Ilihifadhiwa 1 Juni 2013 kwenye Wayback Machine. (Maelfu ya picha na aina ya ajali)
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.