Moto
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Moto ni hali ya kuungua haraka kwa gimba na kutoa joto pamoja na nuru. Kisayansi ni mmenyuko wa kikemia kati ya oksijeni ya hewa na kampaundi za kaboni. Moto ni mfano mkuu wa harakati ya kuoksidisha.



Katika historia ya binadamu matumizi ya moto yalikuwa hatua kubwa ya kujenga utamaduni. Watu hutumia moto kwa kupika, kujilinda dhidi ya baridi na giza, kupeana habari, kuendesha vyombo vya usafiri na kutengeneza umeme.
Moto ni pia jambo haribifuː unaleta hatari kwa mali, afya na maisha ya watu na viumbe vyote.
Remove ads
Moto kikemia
Moto unawaka kama masharti manne yako mahali pamoja:
- gimba lenye uwezo wa kuwaka, kwa kawaida lenye kiasi cha kampaundi za kaboni na hidrojeni
- oksijeni ya kutosha (au: kampaundi za oksijeni)
- chanzo cha joto ya kutosha kwa kuwasha mchanganyiko wa fueli na oksijeni
- mmenyuko mfululizo unaoendeleza hali ya kuwaka kwa moto; huo ni wa lazima kwa kuendelea kwa moto ukihakikisha kuna joto la kutosha kuendeleza moto
Masharti hayo manne huelezwa kwa tetrahedroni ya moto. Hakuna moto kama masharti hayo manne hayapo pamoja.
Moto unazimika kama moja kati ya masharti manne linaondolewa. Katika mfano wa moto wa gesi kwenye jiko la kupikia la gesi moto huu unazimika kwa:
- kuzima gesi ambayo inaondoa chanzo cha fueli
- kufunika moto kabisa maana huko kunazuia oksijeni kufika motoni; baada ya muda mfupi akiba ya oksijeni iliyo karibu na moto huwa imekwisha na moto unazimika
- kumwaga maji juu ya moto; hayo yanapunguza joto motoni haraka sana na harakati ya kuwaka inakwama; kupuliza sana inaweza kuleta tokeo lilelile kwa kuondoa joto kutoka kwa gesi inayoendelea kutoka
- kuingiza kemikali kama halon motoni inayochelewesha mmenyuko ndani ya moto kiasi cha kusimamisha mmenyuko mfululizo.
Remove ads
Moto na utamaduni

Matumizi asilia ya moto
Wataalamu wanaamini kuwa watu wa kale waliona faida ya kutumia moto wa asili unaosababishwa na radi n.k. walipokuta wanyama waliokufa kwenye moto huo nyama yao iliyochomwa kuwa bora kwa lishe kuliko nyama mbichi. Pia walitambua kwamba mimea au sehemu za mimea zilikuwa chakula bora baada ya kukaa motoni kwa muda.
Kwa hiyo, inaaminika kwamba watu hao kwanza walijifunza kubeba moto wa asili na kuudumisha katika nyumba zao, na baadaye walijifunza kuwasha moto wenyewe. Inaaminika kuwa hii ilitokea hata kwa wanadamu wa historia ya awali miaka milioni 0.2-1.8 iliyopita. Hakuna makubaliano juu ya hilo, ingawa ni karibu hakika kwamba lilitokea miaka 500,000 iliyopita. Kuwa na moto karibu na nyumba au mahali pa kulala kulikuwa aina ya ulinzi dhidi ya wanyamapori ambao wanaogopa moto na hawana akili ya kuamua matumizi yake. Moto pia ulisaidia wakati wa kuwinda. Na ilifanya shughuli za usiku au mapangoni ziwezekane. Pia kupika chakula kuliwapa wanadamu lishe tofauti zaidi. Hiyo inamaanisha waliweza kula vitu vilivyopikwa, ambavyo vibichi vilikuwa na sumu, kama vile maharagwe. Moto pia ulifanya iwezekane kwa watu kustahimili baridi na kuhamia sehemu za baridi.
Remove ads
Viungo vya nje
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Moto kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads