Ajeriki

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Ajeriki (pia: Agericus, Airy, Aguy; Harville, karibu na Verdun, Meuse, Galia Kaskazini, leo Ufaransa, 521 hivi - Verdun, 588) alikuwa askofu wa mji huo.

Alijenga makanisa na mabatizio. Pia alisumbuliwa sana na mfalme Theodoriki I kwa sababu aligeuza kanisa lake kuwa kimbilio la waliodhulumiwa [1].

Alisifiwa na rafiki yake askofu Gregori wa Tours [2] na Venansi Fortunati [3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Desemba[4][5][6].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads