Aktini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Aktini (actinium) ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 89 na alama ya Ac . Uzani atomia wa Aktini ni 227.
Aktini ni metali yenye rangi ya fedha. Ni nururifu kiasi cha kung'aa kwenye giza. Hata kiwango kidogo cha aktini ni hatari kwa afya ya watu. Isotopi zake huwa na nusumaisha ya siku chache, isipokuwa 227Ac, inayotokea kiasili katika madini ya urani, ina nusumaisha ya miaka 21.8.
Aktini iligunduliwa mnamo 1899 na Mfaransa André-Louis Debierne. Mnamo 1899, Debierne alielezea dutu hii kuwa inafanana na titani [1] na pia na thori . [2]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads