Almurabitun
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Almurabitun (kutoka Kiarabu: المرابطون, kwa Kiingereza: Almoravids) walikuwa nasaba ya Waberberi [1] kutoka Sahara iliyotawala eneo pana la kaskazini magharibi mwa Afrika na Rasi ya Iberia wakati wa karne ya 11.
Chini ya nasaba hiyo milki yao ilitawala Moroko ya leo, Sahara ya Magharibi, Mauritania, Gibraltar, Tlemcen (leo nchini Algeria) na sehemu kubwa ya nchi ambazo sasa ni Senegal na Mali, pamoja na Hispania na Ureno upande wa Ulaya. Wakati wa kilele chake, milki ilikuwa na upana wa kilomita 3,000 kutoka kaskazini hadi kusini.
Watawala wao walitumia Aghmat (1040-1062) na Marrakech(1062-1147) pamoja na Córdoba kama miji mikuu.
Uvamizi wa Almurabitun upande wa kusini mwa jangwa la Sahara ulikuwa muhimu kwa uenezaji wa Uislamu ukisababisha watawala kadhaa wa Kiafrika kuwa Waislamu, kwa mfano wafalme wa Mali na Dola la Songhai.
Remove ads
Watawala
- Abdallah ibn Yasin (1040-1059)
- Yusuf ibn Tashfin (1061-1106)
- Ali ibn Yusuf (1106-42)
- Tashfin ibn Ali (1142-46)
- Ibrahim ibn Tashfin (1146)
- Ishaq ibn Ali (1146–1147)
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads