Amaury Nolasco
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Amaury Nolasco (Amaury Nolasco Garrido amezaliwa tar. 24 Desemba 1970) ni mwigizaji anayejulikana sana kwa kuigiza kama Fernando Sucre kwenye tamthiliya Prison Break.
Maisha ya awali
Nolasco alizaliwa Puerto Rico, aliposoma baiolojia muda wote katika chuo cha Puerto Rico ili aje kuwa daktari. Kwa ufupi hakuwa na mpango wa kuja kuwa muigizaji. Baada ya kufanya shughuli ndogondogo za uigizaji, Nolasco alihamia New York, ambapo alipata mafunzo katika American British Dramatic Arts.
Rafiki wa utotoni wa Nolasco ni Jorge Posada, walikutana darasa la kwanza. Alifanya kazi kama kwenye klabu moja Los Angeles kama mhudumu.
Remove ads
Wasifu
Punde tu, Nolasco alishiriki katika tamthiliya kadhaa kama vile Arli$$, Crime Scene Investigation na ER. Alishiriki kwa mara ya kwanza kwenye filamu kama Orange Julius kwenye 2 Fast 2 Furious ya Universal. Baadae akashirikia kama Bernie Mac kwenye Mr. 3000.
Pia amecheza kwenye baadhi ya tamthilya na filamu kama George Lopez, CSI: NY na Benchwarmers. Ameuza sura kwenye Mind of Mencia, Aprili 29, 2007. Nolasco ameigiza kwenye filamu Transformers iliyoachiwa kwenye majira ya joto 2007. Lakini amefanya vizauri zaidi na kujitambulisha zaidi baada ya akuigiza kwenye tamthilia Prison Break ya FOX Network.
Nolasco ameuza sura kwenye video ya muziki Yes We Can ya Will.I.Am,[1] ambayo inaonesha kumuunga mkono mgombea urais wa marekani 2008, Barack Obama.
Remove ads
Magizo
Filamu
Tamthiliya
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads