Ameriki

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ameriki
Remove ads

Ameriki ni elementi ya kimetali yenye alama Am na namba atomia 95. Kwenye jedwali la elementi inahesabiwa ndani ya kundi la aktinidi. Ni metali laini yenye rangi ya kijivu-kifedha lakini inaoksidika haraka ikifunikwa na tabaka la oksidi kijivu-nyeusi.


Ukweli wa haraka Ameriki (americium) ...

Ameriki iligunduliwa mwaka 1944 katika maabara ya Chuo Kikuu cha Kalifornia pale Berkeley.

Ameriki ni elementi nururifu ambayo inatokea kiasili kwa viwango vidogo sana, inaundwa ndani ya madini ya urani kutokana mbunguo nururifu asilia ya urani. Nusumaisha ya isotopi zake ni hadi miaka 2,737, hivyo haiwezi kudumu muda mrefu kiasili. Inazalishwa katika tanuri nyuklia na maabara kwa kufyatulia nyutroni kwa plutoni.

Matumizi yake ni hasa katika vigunduzi moshi ambako inatumiwa kwa viwango vidogo ambavyo si hatari kwa afya.

Remove ads

Viungo vya Nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ameriki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads