Amonia

From Wikipedia, the free encyclopedia

Amonia
Remove ads

Amonia ni kampaundi ya nitrojeni na hidrojeni yenye fomula NH3. Ni bidhaa muhimu viwandani. Mwaka 2006, uzalishaji duniani ulifika tani milioni 146.5. [1] Ingawa amonia hupatikana sana katika uasilia na hutumika kila mahali, kemikali hii ni caustic na madhara katika fomu yake isiyochujuka. Katika kaya hutumika kusafisha vyombo.

Thumb
Amonia molekuli

Karibu 80% ya amonia inayozalishwa duniani hubadilishwa kuwa mbolea za sintetiki kama vile nitrati ya amonia, fosfeti za amonia, salfeti ya amonia, urea na nitrati ya amonia ya kalsiamu. Amonia huzalishwa leo kwa kutumia mchakato wa Haber-Bosch unaotoa hidrojeni kutoka kwa malighafi ya visukuku (gesi asilia au makaa ya mawe), na kusababisha uzalishaji wa CO2. Amonia inayoweza kutumika tena inaweza kutayarishwa ikiwa hidrojeni itatolewa kutokana na mgawanyiko wa maji ya kielektroniki kwa kutumia umeme unaoweza kutumika tena (nishati ya jua na upepo). Afrika ina uwezo mzuri wa kutoa amonia inayoweza kutumika tena na kupunguza utegemezi wa uagizaji wa mbolea[2][3][4].

Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads