Azori
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Azori (kwa Kireno: Ilhas dos Açores - Visiwa vya vipanga) ni funguvisiwa la Ureno lenye visiwa tisa vikubwa na vingine vidogo katika Atlantiki takriban km 1,500 magharibi ya Ulaya na 3,600 mashariki ya Amerika ya Kaskazini.
Ni jimbo la kujitawala la Ureno (Região Autónoma dos Açores) na sehemu ya Umoja wa Ulaya.
Visiwa vyote ni vya asili ya kivolkeno; hali halisi ni vilele vya milima mirefu sana vinavyotoka nje ya maji kutoka sakafu ya bahari. Milima hiyo ni sehemu ya mgongo kati wa Atlantiki yanapokutana mabamba ya gandunia ya Amerika ya Kaskazini na Afrika.
Mlima Pico kwenye kisiwa cha Pico ni mlima mrefu wa Ureno wenye kimo cha m 2,351 juu ya UB.
Visiwa viligunduliwa na mabaharia Wareno mwaka 1427: vilipatikana bila wanadamu. Wakazi wa kwanza walifika kutoka Ureno mwaka 1439.
Remove ads
Viungo vya nje
- Azores Info Ilihifadhiwa 9 Januari 2016 kwenye Wayback Machine.
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Azori kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads