Bahari ya Eire

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bahari ya Eire
Remove ads

Bahari ya Eire (kwa Kiingereza: Irish Sea) ni sehemu ya bahari inayotenganisha visiwa vya Eire (Ireland) na Britania.Ina visiwa viwili vikubwa kiasi ambayo ni Anglesey (Welisi) na Isle of Man, pamoja na visiwa vidogo. Inapakana na nchi za Welisi, Uingereza na Uskoti (zote sehemu za Ufalme wa Muungano) upande wa mashariki, halafu Eire na Eire ya Kaskazini (pia sehemu ya Ufalme wa Muungano) upande wa magharibi.

Thumb
Ramani ya Bahari ya Eire (Irish Sea).

Kila mwaka kuna abiria milioni 12 wanaovuka bahari hii na bidhaa tani milioni 17 zinasafirishwa kati ya Britania na Eire.

Remove ads

Uchumi

Eneo lake ni kilomita za mraba 46,007. Kina kirefu kinafikia mita 300 lakini kwa wastani ni mnamo mita 50[1].

Uvuvi ni biashara muhimu, mwaka 2008 samaki tani 38,000 walikamatwa [2].

Chini ya bahari hii kuna akiba za mafuta na gesi pamoja na vituo vya kuchimba maliasili hizi[3].

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads