Ramani

uwakilishi wa kuona wa nafasi ya dhana; taswira inayosisitiza uhusiano kati ya vipengee vya nafasi fulani, kama vile vitu, maeneo au mada. From Wikipedia, the free encyclopedia

Ramani
Remove ads

Ramani ni picha - kwa kawaida mchoro - ya dunia au sehemu au sifa zake.

Thumb
Ramani ya dunia ya mwaka 1662
Thumb
Ramani yaonyesha kilele cha mlima Kilimanjaro na mistari ya kimo
Thumb
Ramani ya muundo wa usafiri wa reli ndani ya mji wa London, Uingereza

Ni tofauti na picha iliyopigwa kwa kamera kutoka ndege au chombo cha angani kwa sababu mchora ramani anachagua anachotaka kuonyesha na kuzipa uzito sifa anazotaka kuziwekea mkazo.

Kuna aina nyingi za ramani:

  • ramani za topografia huonyesha sura ya nchi (kwa mfano: bahari, nchi kavu, milima, mito, kimo cha ardhi na kina cha bahari)
  • ramani za idadi huonyesha sifa fulani kuhusiana na dunia (kwa mfano: historia, uchumi, mtawanyiko wa wakazi katika nchi n.k.)
  • ramani inaweza kufuata sura ya nchi
  • ramani inaweza kufuata mahitaji ya msomaji (ramani ya njia ya reli huonyesha mstari tu na mfuatano wa vituo bila kutaja kona na mabadiliko ya mwelekeo)

Kila mchoraramani anahitaji kuchagua jinsi ya kuonyesha mambo yake. Kwa ramani za kijiografia tatizo hutokana na umbo la dunia ambalo ni tufe wakati ramani kwa kawaida ni karatasi bapa.

Remove ads

Viungo vya nje

Ukweli wa haraka
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads