Ban Ki-moon
Mwanasiasa na mwanadiplomasia wa Korea Kusini From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ban Ki-moon (* Eumseong, Korea, 13 Juni 1944) alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa tangu tarehe 1 Januari 2007 hadi 31 Desemba 2016 akimfuata Kofi Annan.[1]


Ban aliwahi kuwa Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini kati ya miaka 2004 na 2006. Tarehe 13 Oktoba 2006 alichaguliwa na Mkutano Mkuu wa UM kuwa Katibu Mkuu.
Mwaka 2013, jarida la Fobres la nchini Marekani lilimtaja Ban kuwa mtu wa 32 mwenye nguvu duniani na kuwa wa kwanza katika Korea Kusini. Mwaka 2014 alitajwa kuwa mtu wa tatu mwenye nguvu Korea Kusini baada ya Lee-Kun hee na Lee-jae yong.
Remove ads
Elimu
Ban alisoma katika Korea Kusini hadi digrii ya kwanza ya B.A. kwenye chuo kikuu cha Seoul (1970). Mwaka 1985 aliongeza digrii ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Harvard (Marekani).
Familia
Ban alioa mke aitwaye Yoo Soon-taek na kuzaa mvulana mmoja na mabinti wawili. [2]
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads